Kupitia Mashindano ya Drafti yaliyoratibiwa chini ya Afisa Tarafa wa Nyaishozi Bw. Kelvin Berege, Kata ya Nyaishozi Mkoani Kagera imezibwaga Kata zingine 3 za Tarafa hiyo Yani Rugu, Nyakasimbi na Ihembe kwa kuibuka kidedea na kujinyakulia zawadi ya mbuzi aliyenona siku ya Jumamosi tarehe 04/10/2025.
Mashindano hayo yalishirikisha washiriki wanne toka kila kata, na mwitikio wa washiriki na wananchi ulikuwa mkubwa uliojaa hamasa kubwa ya hali ya juu, kwani pia kulikuwa na Kahawa, Tangawizi na Karanga za bure kwa washiriki wote.
Kupitia Mashindano hayo Afisa Tarafa Bw. BEREGE, alifikisha ujumbe kwa wananchi juu ya Ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya Wilaya ya Karagwe mnamo tarehe 16/10/2025.
Lakini pia kutoa Elimu ya Mpiga Kura juu ya kuitunza tunu yetu ya Amani na Utulivu kipindi hiki cha uchaguzi, na kuwataka wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba ya kujitokeza kupiga kura kwa amani hapo 29 OkToba ✅.
Bw. Berege alimaliza kwa kusisitiza pia hatoishia hapo juu ya uratibu wa michezo mbalimbali, kwani baada ya Bonanza la watumishi lililofanyika Novemba mwaka jana, likaja Bonanza la Mashabiki wa Simba na Yanga April 2025, limeisha hili la drafti, yanakuja mengine mengi ili kuzidi kuwaleta wananchi karibu kupitia michezo na Hamasa mbali mbali.
Uchaguzi Mkuu 2025 : “ Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura ✅
Imetolewa :
Kelvin Erick Berege
Afisa Tarafa – Nyaishozi.
Related