Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amemuomba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka wananchi wa Wilaya ya Sengerema, hususan Jimbo la Buchosa, katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami akisema ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili wakazi wa eneo hilo wakati wa usafiri.
Aidha, Shigongo alitaja pia tatizo la uhaba wa umeme kuwa changamoto nyingine inayowakwamisha wananchi katika shughuli zao za kiuchumi.
Shigongo aliyasema hayo leo katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika katika Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
Related