DK.BASHIRU ASEMA DK. SAMIA ANA UWEZO MKUBWA KUYAKABILI MAJARIBU NA NCHI IKO SALAMA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mwanza

KATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally amesema mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan katika miaka minne ya uongozi wake licha ya kuchukua uongozi katika kipindi kigumu lakini amefanikiwa kuiweka nchi kuwa salama na ameshinda majaribu mengi.

Hata hivyo amesema kelele zinazopigwa mitandaoni zisipuuzwe lakini pia ziangaliwe kwa umakini huku akieleza wazi binafsi ana matumaini makubwa na vijana wa Taifa la Tanzania akımtolea mfano Waziri wa Maji Jumaa Aweso na kusisitiza kwa mtazamo wake haoni kijana anayeweza kuvuruga amani ya Taifa hili kwani wengi ni vijana wema.

“Umekiandaa vizuri chama chetu na nchi kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Ndio maana wananchi wanakusikiliza kwa utulivu. Nimesikia maneno hasa vijana kuhusu uwezo wa mgombea wetu kiuongozi, ninawahakikishia amepatwa na majaribu amejaribiwa na amevuka salama. 

“Nataka kuzungumzia  uwezo wa mgombea wetu Dk.Samia Suluhu Hassan, nasikia maneno hasa kutoka kwa vijana kana kwamba wana wasiwasi  hivi.Nawahakikishia huyu kiongozi wetu ambaye anaomba ridhaa tena amekutana na majaribu, ameshajaribiwa na ameshinda majaribu Kwahiyo tunaunakika tutavuka salama 

“Kama nchi yetu imebaki nchi moja na Chama chetu kimeendelea kuwa kimoja , usalama na amani umetamalaki katika kipindi kigumu cha mabadiliko ya Serikali yaliyotokea hafla tumevuka.

“Hızı rabsha rabsha ambazo zinafanywa maana lile tukio halijapangwa lakini aliweza kuikabili wakati huo huo akiwa kwenye kiti hivi vingine vinawatu wamevipanga ni rahisi kuvidhibiti.Simaanishi tupuuze majaribio ya kutikisa amani ya nchi yetu hata kidogo.

“Simaanishi kwamba tupuuze jaribio la kutikiza na kuvuruga misingi ya amani yetu .Ninachotaka kusema huyu kiongozi ni hazina ya uzoefu wa uongozi katika vipindi vigumu sana na mimi sina mashaka kwasababu watanzania waliompa ushirikiano ndio hao hao hawajabadilika 

“Watanzania waliomuombea dua ndio hao hao wanaendelea kumuombea kura , watanzania ambao wanatangaza kazı njema aliyoifanya kwa miaka minne na nusu ndio hao hao ambao anawaongoza.

“Sasa watanzania wakuvunja amani watatoka wapi tusipuuze lakini tusiendekeze mambo ambayo yanayoweza yakatutoa kwenye mstari wa kujenga Taifa letu,”amesema Dk.Bashiru alipokuwa akielezea uwezo wa Dk.Samia katika kukabiliana na majaribio mengi ambayo ameyashinda.

Katika hatua nyingine Dk.  Bashiru amemsifia Dk. Samia kwa dhamira yake ya kufufua Vyama vya Ushirika huku akifafanua kuwa ni sehemu ya ukuaji uchumi hasa kwa wakulima na wafanyabiashara wadogo.

“Kufufua vyama vya Ushirika ni uamuzo wa busara, hawa wananchi wa Mwanza wana historia wanajua vyama vya Ushirika vilileleta ukombozi wa nchi. Kanda hii maendeleo makubwa yalifikiwa kiuchumi kwa sababu ya Ushirika.

“Kwa muda mfupi umefufua Ushirika na kuanzisha Benki ya Ushirika na mifumo imeimarishwa. Ninaamini kujiunga katika vyama vya Ushirika ndio kufanikiwa kwa wakulima na wanaofanya shughuli ndogondogo.

Ameongeza kuwa  Kanda ya Ziwa shughuli kubwa ni uvuvi, mifugo, kilimo na madini. Hata shughuli nyingine za kiuchumi zinategemea maeneo hayo.

“Ilani ya CCM inagusia kuanziahwa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi. Itatusaidia kuratibu, usimamizi  utafiti na maendeleo ya sekta hiyo. Kilimo ni chakula, kilimo ni ajira  kilimo ni usalama wa nchi. 

“Mwalimu Nyerere alipoingia madrakani mwaka 1962 alikuta nchi inakabiliwa na njaa, alikuwa muumini wa kujitegemea lakini kwa fedheha kubwa akaenda  kuomba msaada nchi za Magharibi.

“Akapewa msaada wa Mahindi ya Njano. Akaanzisha programu za kilimo cha kufa na kupona na siasa ni kilimo. Wewe Sk. Samia tangu uingie madarakan nchi ina chakula na ziada ya chakula,” amesema.