MRADI WA EACOP WANYANYUA UCHUMI WA TAIFA

 

Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umewezesha kukua kwa uchumi haswa katika mikoa ambayo imepitiwa na bomba hilo.

Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhe. Balozi Ombeni Sefue.

“Mradi huu umekua na manufaa makubwa katika nchi yetu kwanza tumeona mradi umelipa fidia nzuri hii ikijumuisha nyumba, viwango vizuri vya pesa, chakula na elimu ya kilimo na ufugaji pamoja na pembejeo”, amesema Mhe. Balozi.

Mhe. Sefue amefafanua zaidi kuwa kwa sasa maisha ya wananchi yameimarika na wanaendesha shughuli zao za kilimo na ufugaji kwa ufanisi zaidi.

Aidha Mhe. Balozi amebainisha kuwa pamoja na ustawi wa uchumi, mradi umefanikiwa kuweza kufuata misingi bora ya utunzaji wa mazingira na kwa sasa ni moja ya miradi bora duniani katika utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Burian amethibitisha mchango mkubwa unaofanywa na EACOP katika kujenga uchumi na ustawi wa mkoa wa Tanga.

“Sisi Kama Mkoa wa Tanga kwanza tunashukuru sana na kupongeza serikali yetu kwa kuwezesha mradi kuwa nchini lakini unionize TPDC kwa usimamizi bora wa mradi kwakweli mradi umeijenga Tanga”, ameeleza Mkuu wa Mkoa.

Mhe. Batilda amefafanua kuwa moja ya sehemu ambayo imekua kwa kasi kutokana na mradi huu ni ukuaji wa Shughuli za Bandari ambapo kwa sasa tunapokea Mel zaidi ya 50 kwa mwezi.

Mhe. Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa kwa sasa mradi unashirikiana na TANESCO Ili kuweza kusambaza umeme kwenye vijiji ambavyo havina umeme katika maeneo yaliyopitiwa na bomba hilo.

Aidha katika masuala uwajibikaji wa Jami ‘CSR’ mradi unatarajia kujenga kituo bora cha afya ili kuboresha huduma za afya kwenye mkoa wa Tanga.

Baada ya kumalizia kikao na Mkuu wa Mkoa wa Tanga walipata wasaa wa kutembelea shughuli za ujenzi wa mradi katika eneo la mto Sigi ambapo bomba linapitishwa zaidi ya mita 15 chini ya sakafu ya mto kwa kutumia teknolojia ya HDD.

Pamoja na ujenzi wa bomba katika Mkoa wa Tanga, mradi unajenga matenki ya kuhifadhia mafuta, kituo kituo kikuu pamoja na ghati.