Mwanaume mmoja (Tatizo Yohana Mzumbwe) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mama yake wa kambo katika tukio lililotokea mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, tukio hilo lilitokea baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia uliodaiwa kuibuka kati ya mtuhumiwa na marehemu.
“Ni kweli tunamshikilia kijana mmoja kwa tuhuma za kumuua mama yake wa kambo. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na mvutano wa kifamilia uliosababisha vurugu na hatimaye kifo cha marehemu,” alisema Kamanda huyo.
Related