CHANZO CHA IBRAHIM MAFIA KUPIGWA NI MAKOCHA WAKE

 :::::::

Bondia Ibrahim Mafia kisima kapigwa TKO raundi ya nne ya pambano na mfilipino Alvin Camique kwasababu ya makocha wake.

Bila ya kuwakosea heshima makocha wa Ibrahim Mafia ambao walishiriki kumpa maelekezo wakati wa pambano lakini ukweli mchungu wao ndio walio changia Mtanzania mwenzetu kupigwa.

Kwanza ukitazama wakati anapigwa ngumi ya kwanza ambayo Ibrahim Mafia alisetiwa na ‘jab’ iliyopenya kwenye gadi yake akashusha ‘jab’ ambayo ni ngumi yake ya kushoto ikatoka kwenye eneo lake ndipo hapo akanaswa kwenye mtego na mfilipino.

Baada Ibrahim kuishuhaa ‘jab’ yake ili ampige ‘right upper cut’ mpinzani wake na yule mfilipino akili yake ilifanya kazi kama umeme chap akamtandika ‘right upper cut’ Mafia ambayo ilimlewesha baadae akasindikizwa na ngumu nyingine palepale kwenye eneo la katikati ya jicho na sikio lake la kushoto.

Ibrahim Mafia alishaona haya ni maji marefu siyawezi ndomana alikua anafosi sana ampige ‘KO’ mfilipino kwa kuijaribu ‘right upper cut’ mara kadhaa lakini alimkosa pia akajaribu mbinu nyingine ya kushindana nae nguvu mpinzani wake kitu ambacho nacho ndicho kilikua kbaya zaidi.

Haya turudi kwa makocha wake wamechangia vipi kupigwa kwa Ibrahim Mafia ni kushindwa kumsoma mpinzani wao alivyokua akicheza kwasababu Mfilipino ana nguvu pia ana ngumi nzito maana ukitaka kuamini jamaa ana ngumi nzito ni pale yeye akipigwa inakua poa anazimeza ngumi lakini akimpiga Ibra basi Ibra anatikisika haswa.

Na kuhusu nguvu alikua muda wote anabadilishana ngumi na kushindana ubavu na Ibra bila ya yeye kutetereka hata ukimtazama ‘footwork’ yake ilikua imara kiasi alianza na kumaliza na kasi ileile hadi alipompiga Ibra ‘TKO’.

Sasa kwa namna hiyo ya upiganaji wa yule mfilipino ilibidi makocha wa Ibra wampe mbinu ya kubadili mchezo aacha kushindana nae nguvu na kuacha kulazimisha waipate ‘KO’ kwa mpinzani mgumu kama yule ila walitakiwa kumwambia awe ana ‘score’ na kutembea yaani anapiga ngumi muhumu zenye madhara kwa mfilipino kisha anatembea na hata wakipata ushindi wa ‘points’ ni sawa ila makocha wa Ibra waliishiwa nguvu na wao wakawa kama watazamaji wa kawaida tu wasijue nini wafanye ili bondia wao asikandwe.