Junza wa tamthilia ya Mpali afariki dunia

Lusaka. Muigizaji maarufu kwenye tamthilia ya Mpali ya Zambia, maarufu kwa jina la Junza, aliyekuwa akiigiza kama mke mkubwa wa Nguzu, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Televesheni ya Taifa ya Zambia, Junza Mabaye ambaye jina lake halisi ni Wanga Zulu, amefariki dunia Alhamisi Oktoba 9, 2025 katika Hospitali ya Mafunzo ya Levy Mwanawasa baada ya kuugua.

Mwigizaji huyo ambaye kwenye uigizaji kama mke mkubwa wa Nguzu mwenye wake saba, kwenye filamu ya Mpali pia alifahamika kama mama wa Hambe, mtoto wa kiume aliyelelewa na Nguzu.

Endelea kufuatilia Mwananchi.