Mwandishi Daniel Mbega afariki dunia, TEF wamlilia

Dar es Salaaam. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeatangaza kifo cha mwanachama wake, Daniel Mbega, aliyefariki dunia leo, Jumamosi, Oktoba 11, 2025, katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Taraifa hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Balile amesema kwa mujibu wa taarifa za familia, Mbega alizidiwa  saa 10 alfajiri na alipelekwa Hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu, ambako alipoteza maisha wakati madaktari wakiendelea kumhudumia.

“Daniel Mbega alikuwa mwandishi wa habari mwenye uzoefua wa zaidi ya miaka 20 katika nyanja ya uandishi wa habari za uchunguzi (investigative jouralism).

“Ameshafanya kazi katıka vyombo mmalimbali vya habari nchini na kuchangia kwa kiasi kikubwa kukuza tasnia ya hahari nchini,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Mbega Elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi Chigwingwili, wilayani Kongwa mkoani Dodoma. Baadaye alıjiunga na Shule ya Sekondari Pugu, kabla ya kucndelea na mafinzo ya uandishi wa habari katika cluo cha Tanzania School of Joumalism (TSJ).

Ameongeza kuwa hadi unauti unamkuta, Mbega alikuwa mwanachama hai wa TEF, akitambulika kwa mchango wake wa kitaaluma, mandili ya kazi, na kujitolea katika kuendeleza misingi ya uhuru wa vyombo sya haburi achini.

Mwili wa marchemu unaagwa kesho, Jumapili Oktoba 12, 2025, katika Hospitali ya Temeke, kabla ya kusafirishwa kwenda Chigwingwili, Kongwa – Dodoma kwa ajili ya maziko yanayotarajiwa kufanyika Jumatatu.

“TEF inaungana na familia, ndugu, jamaa, marafiki na waandishi wa habari wote nchini katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Tunatoa pole za dhati kwa fumilia ya marehemu na tunamuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,”imesema taarifa hiyo.