Alichokisema Wenje baada ya kutimkia CCM

Geita. “Kwa umati huu nimeamini Oktoba tunatiki”.Hiyo ni kauli ya kwanza ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Kanda ya Ziwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Ezekiah Wenje  baada ya kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wenje ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Nyamagana kwa tiketi ya Chadema, amehama chama hicho leo Jumatatu Oktoba 13,2025 mbele ya Rais na mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa kampeni wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Akizungumza baada ya kuhamia chama hicho, Wenje amesema kazi ambayo CCM imefanya tangu Taifa lipate uhuru ni  pamoja na nchi kuwa na amani na utulivu, “amani, utulivu na maendeleo ni pacha lazima viende pamoja.”

Amesema madai ya Chadema kuzuiwa na Serikali kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025 siyo ya kweli ni uongo na ni suala linalopaswa kupuuzwa kwani waliamua wenyewe kukataa kushiriki uchaguzi.

Endelea kufuatilia Mwananchi.