DK.SAMIA AANIKA MPANGO WA KUJENGA UWANJA MKUBWA WA KISASA GEITA MJINI

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Geita

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ameahidi katika miaka mitano ijayo Serikali itajenga kiwanja kikubwa cha michezo Geita mjini mkoani Geita.

Akizungumza leo Oktoba 13,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Jimbo la Geitq Mjini katika Uwanja wa EPZA Bombambili mkoani Geita Mgombea Urais Dk.Samia amesema katika katika kukuza utamaduni, sanaa na michezo Serikali imeanza ujenzi wa viwanja vikubwa vya michezo.

Amefafanua kwamba mchezo wa mpira wa miguu Serikali inaendelea  kujenga uwanja Bukombe na kwa Geita Mjini pia utajengwa Uwanja mkubwa wa kisasa.

Pamoja na mambo mengine Mgombea Urais Dk.Samia amesisitiza kwamba Serikali yake itaendelea kuwekeza kwenye michezo kwani sekta  hiyo inatoa ajira nyingi kwa vijana.