WENJE OKTOBA ANA TIKI KWA DK SAMIA,AREJEA CCM NA KUTOA KAULI

 Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chato 

EZEKIA Wenje Oktoba 29 naye anatiki kwa Dk.Samia Suluhu Hassan ! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya leo Oktoba 12,2025 Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje kutangaza kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ujio wa Wenje ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Nyamaga ni pigo kubwa kwa CHADEMA kwani alikuwa ni miongoni mwa wanasiasa mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama hicho.

Wenye ni moja ya viongozi wa CHADEMA waliokuwa na nguvu na kwa Jiji la Mwanza alikuwa amtengeneza utawala wake na hakuna aliyekuwa akiamini kama iko siku atasimama katika Jukwaa la CCM akiwa lakini hakuna lisilo na mwisho na leo amefungua ukurasa mpya baada ya kuachana nq CHADEMA na Şaş’a anasubiri Kutiki kwa Samia.

Akizungumza na maelfu ya wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mgombea Urais kupitia CCM Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wilayani Chato mkoani Geita, Wenje alisema CCM imefanyakazi kubwa ya maendeleo nchini.

Amesema kwamba wakati anasoma shule ya sekondari walikuwa wakitumia saa 10 kusafiri kutoka Mwanza hadi Geita lakini sasa wanatumia saa mbili pekee.

Wenje ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema  siyo kweli kwamba serikali imewazuia kushiriki uchaguzi mkuu.

Hata hivyo Wenje ametumia nafasi hiyo kuelezea Kamba hakuna taifa lolote duniani ambalo limepata maendeleo yanayochipua kama uyoga bali maendeleo ni mchakato na kutoa mfano hata Marekani ambayo imepata uhuru wake miaka 250 iliyopita lakini bado inakabiliwa na changamoto ya ajira.

Uamuzi wa Wenje kuamua kuhamia Chama Cha Mapinduzi inaongeza idadi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani ambao wakmeamua kujiunga katika Chama hicho hasa katika kipindi hiki ambacho mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan ameendelea kuomba kura pamoja na kuinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030.

Zipo sababu nyingi ambazo zimewafanya wapinzani kujiunga CCM na moja ya sababu hizo ni namna ambavyo Dk.Samia Suluhu Hassan alivyoweza kuliongoza Taifa la Tanzania katika misingi ya maridhiano sambamba na kuboresha maisha ya Watanzania kupitia sekta mbalimbali.