Binti wa Eminem, Alaina Scott, Atangaza Ujauzito – Global Publishers



Alaina Scott, binti wa rapa maarufu duniani Eminem, ametangaza kuwa anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mume wake, Matt Moeller.Marshall Mathers anaejulikana kama Eminem, alimlea Alaina kama binti yake tangu akiwa mdogo. Alaina ni mtoto wa Dawn Scott, ambaye ni dada wa Kim Scott, mke wa zamani wa Eminem.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Alaina aliandika kwa hisia kali:“Mchanganyiko bora wa mimi na wewe. Kwa miezi kadhaa nimebeba mapigo madogo ya moyo tumboni mwangu… sijawahi kujisikia mwenye shukrani kama hivi kwa zawadi hii ya kipekee na nafasi ya kukuza familia yetu.”

Alaina na Matt walifunga ndoa mwaka 2023, na tangazo hili limepokelewa kwa pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki na marafiki wao.

Marshall Mathers anaejulikana kama Eminem, alimlea Alaina kama binti yake tangu akiwa mdogo. Alaina ni mtoto wa Dawn Scott, ambaye ni dada wa Kim Scott, mke wa zamani wa Eminem.