DC MWANZIVA ASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA RUTAMBA AKIHAMASISHA WANANCHI KUJITOLEA.

Mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva ametoa raiĀ  kwa wananchi wa Wilaya hiyo kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kujitolea kwenye miradi inayoletwa na serikali kwenye maeneo yao ili ikamilike kwa iwakati na kutoa huduma za uhakika.

Mwanziva ametoa rai hiyo leo Oktoba 14,2025 alipozungumza na wananchi wa kata ya Rutamba kupitia ziara yake ya kuhamasisha wananchi wa kata hiyo kushiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya Rutamba chenye thamani ya shilingi 666,233,935.00.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi ametuma fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo hayo ambayo yanaenda kurahisisha huduma muhimu ya Afya kwa wanaRutamba.

Aidha,amewasisitizaWasimamizi wa miradi ya maendeleo Wilayani humo kuhakikisha inakamilika kwa wakati kulingana na thamani ya fedha iliyowekwa kwenye miradi hiyo kwa kuzingatia ubora wa hali ya Juu.