Gabon; Kiongozi wa Kijeshi Atangaz Kugombea Urais – Global Publishers



kiongozi wa kijeshi wa Gabon Brice Oligui Nguema

Takriban miaka miwili baada ya kuongoza mapinduzi yaliyomaliza utawala wa familia ya Bongo uliodumu kwa zaidi ya nusu karne, kiongozi wa kijeshi wa Gabon Brice Oligui Nguema ametangaza kugombea urais katika uchaguzi utakaofanyika Aprili 12.

Nguema, mwenye umri wa miaka 50, alitangaza uamuzi huo jijini Libreville, akisema ana ndoto ya kuona “Gabon ikiinuka kutoka majivuni.” Baada ya kumng’oa madarakani Rais Ali Bongo mwaka 2023, Nguema alikuwa ameahidi kurejesha mamlaka kwa raia baada ya kipindi cha mpito.

Bunge la mpito lililompa ruhusa mwezi Januari lilipitisha sheria mpya ya uchaguzi inayoruhusu wanajeshi na mahakimu kugombea.
Kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa Infos CTRI Officiel, Nguema atalazimika kuachia wadhifa wake wa sasa wakati wa kampeni, na iwapo hatashinda, “atarudi kambini.”