MRADI WA UTAFITI WA UCHIMBAJI MAFUTA NA GESI WAFIKIA PAZURI

Na.Ashura Mohamed-Karatu 

Naibu katibu Mkuu wizara ya Nishati bw.Dkt.James Mataragio  ameridhishwa na kasi ya  mradi  mradi wa utafutaji mafuta na gesi asilia kitalu cha EYAS WEMBERE kilichopo karatu mkoani  Arusha.

Ziara hiyo ya Naibu katibu mkuu inaeleza kuwa  mradi huo ambao ni mkakati maalum wa serikali ya Awamu ya sita na pia unatajwa iwapo utakamilika na mafuta kupatikana  utalisaidia taifa kuokoa fedha nyingi za kigeni na kuwezesha nchi kupata maendeleo badala ya fedha hizo kutumika kwenye kuagiza mafuta nje ya nchi.

Akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya kutembelea mradi huo  ambao unalenga kutafuta mafuta na gesi katika bonde la Ufa la Afrika Mashariki Dkt.Mataragio alisema kuwa mradi huo ulianza mwaka 2015 ulianza kwa kukusanya data mbali mbali ambazo zinahusiana na mafuta na gesi katika eneo hilo.

“Awamu ya kwanza mradi huu tulianza kukusanya data  kwa kutumia ndege yaani na baada ya hapo tulikusanya data zingine ambazo zilikuwa zinahusisha na  uchorongaji visima vitatu katika maeneo ya Singida ,Simiyu na Tabora zilibainisha miamba tabaka ambayo Ina mafuta  kwahiyo tukajiridhisha kuwa katika Eyas Wambele Kuna miamba ambayo inaweza kihifadhi Mafuta mbapo iligharimu kiasi Cha shilingi bilioni nane,kwa shughuli hizo na kazi hii ilifanywa na Shirika letu la Mafuta ambalo ni  (TPDC).”Alisema Dkt.Mataragio

Aidha alibainishi kuwa Awamu ya Pili ilihusisha ukusanyaji wa data Mtetemo kuangalia kina Cha miamba tabaka, kwa sababu asili ya mafuta ni lazima uwe na kina kiasi Fulani ili uweze kupata mafuta au lah ambapo shughuli hiyo unafanya na kampuni ya kitanzania ya African Geophysical  Services (AGS).

Pia amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya  Africa Geophysical Service (AGS),kuharakisha kasi ya mradi ikiwa ni pamoja kuongeza rasilimali watu ili mradi huo uweze kukamika  ndani ya wakati uliopangwa.

“Katika Zoezi hili  Awamu hii hili la kukusanya data Mtetemo lilifanyika kwa Awamu mbili Awamu ya kwanza tulichukua data za 2D za size na zilikuwa na urefu wa kilometa 260 kilometa na tulitumia kiasi Cha shilingi zaidi ya bilioni 10,ambapo baada ya kukamilika tulikuja katika Awamu  ya pili  ya uchukuaji wa data mitetemo ambayo ndio hii na tumeshaikamikisha kwa asilimia 47, na tumeshachukua kiasi Cha data kilometa 430,na itagharimu bilioni 45 kazi inaendelea na kama mnavyoona vifaa vipi imara kuhakikisha mradi huu utakamilika na kuleta matokeo chanya kwa nchi.”Alisisitiza Dkt.Mataragio

Dkt.Mataragio alisema kuwa huo ni  mradi muhimu kwa serikali kwa kuwa kama mafuta yatagundulika basi nchi itaweza kuokoa fedha za kigeni ambazo hutumika kununua mafuta nje ya nchi na umeajiri watanzania zaidi ya 500.

Kwa Upande wake Mwenyekiti bw.Salim Ajib  Mwenyekiti wa kampuni  ya AGS alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa taifa na kampuni hiyo pia ambapo wameongezeka wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa kazi inafanyika kwa ufanisi ili kuweza kutoa data nzuri sana na kuweza kupata mafuta na kuhakikisha nchi inaendelea.

Pia alitumia fursa hiyo kusema kuwa kampuni hiyo Ina mchango katika eneo hilo kwa kuwa inawawezesha kupata ujuzi Vijana wa kitanzania pindi nmradi utakamilika.

Bwana Pastory  Maduka Mkazi wa Mwanza ambaye anafanya kazi katika eneo hilo alieleza kuwa uwepo wa mradi huo ni fursa kwao kama Vijana ambapo unawawezesha kupata ujuzi na kipato kinachowawezesha kujikimu wao na familia zao.

Mjiolojia Paschal Njiko ni kaimu  Mkurugenzi wa Utafutaji Uendelezaji na Uzalishaji kutoka  TPDC alisema kuwa Shirika hilo lina jukum la  kufanya Utafiti wa Mafuta na Gesi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na katika eneo hilo wanashirikiana na kampuni ya AGS,katika kutekeleza hilo ili kupata Taarifa za kina ili kuendelea na Zoezi linalofuata la uchimbaji Visima virefu vya Mafuta.

“Wenzetu nchi za jirani Kenya na Uganda walishafanya tafiti na kugundua mafuta katika maeneo yao ya bonde la Ufa sisi Tanzania ndio tulikuwa tumebakia nyuma na sasa  TPDC kama Shirika la Taifa  tumeamua katika  mabonde yetu ya Ufa haswa hili la Upande wa Mashariki  tuendele na utafiti wa kina na tuone kama tunaweza kuchimba mafuta au lah ila kwa kutumia data za kampuni hii ya AGS dalili ni kubwa na tunaweza kufanya maamuzi makubwa hapo baadae ndani ya miaka miwili ijayo.”Alisema Njiko

Kwa upande wake, mmoja wa wanufaika wa  mradi wa Bonde la Eyasi Wembere, Biru Benjamini alisema kuwa kupitia mradi huo wameweza kunufaika na elimu,ujuzi na utaalamu ikiwa ni pamoja na kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.

Mradi huo  unatarajiwa kumalizika April 2026 ambapo ambapo naibu katibu mkuu ametaka kasi ya utekelezaji wa shughuli za mradi unaharakishwa ili kumalizika ndani ya kipindi kilichopangwa.

Mradi huo wa utafiti wa uchimbaji wa mafuta na gesi unahusisha mikoa ya Arusha,Manyara,Tabora,Singida na Simiyu