Poshy Queen Aibua Gumzo Mitandaoni Kwa Kumposti Mpenzi Mpya – Global Publishers



Mrembo maarufu wa mitandao ya kijamii, Poshy Queen (@poshyqueeen), ambaye pia ni mke wa mfanyabiashara maarufu anayejulikana kama Dalali, ameibua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kumposti mpenzi wake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram leo.

Picha iliyosambaa kwa kasi kwenye mtandao huo inaonyesha Poshy Queen akikumbatiwa kwa mapenzi na mwanaume huyo, lakini sura yake imefichwa kwa makusudi. Kitendo hicho kimeibua maswali na uvumi miongoni mwa mashabiki wake kuhusu hali yake ya mapenzi na maisha ya kibinafsi.

Mashabiki wengi wametoa maoni mchanganyiko; wengine wakimpongeza kwa “kupata furaha mpya,” huku wengine wakitaka aeleze ukweli kuhusu mpenzi wake, wakisema huwezi kuendelea “kuficha kila kitu mtandaoni.”