Washindi wa Absa GirlCode Hackathon 2025 wapongezwa

Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Emanuel Mwinuka ( wa nne kushoto) akizungumza na washiriki wa programu iliyopewa jina la ‘Absa GirlCode Hackathon 2025’ ambapo  wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali  zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia  sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo ya Kibenki ya Absa, Bi. Rose Mwingira.Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya ( wa pili kulia ) akikabidhi cheti kwa washindi wa kwanza, Kikundi cha Tokiva Sisters wakati wa programu iliyopewa jina la ‘Absa GirlCode Hackathon 2025’ ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla  iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki hiyo, Bw. Oscar Mwamfwagasi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Emanuel Mwinuka.Mkurugenzi wa Flo Pads, Bi.Flora Njelekela ( kulia ) akikabidhi cheti kwa washindi wa pili kikundi cha Code Crafters wakati wa programu iliyopewa jina la ‘Absa GirlCode Hackathon 2025’, ambapo  wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali  zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia  sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Oscar Mwamfwagasi ( kulia ) akikabidhi cheti kwa washindi wa tatu kikundi cha Tech Divas wakati wa programu iliyopewa jina la ‘Absa GirlCode Hackathon 2025’ ambapo  wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali  zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia  sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (katikati), akizungumza na baadhi ya washiriki wa programu ya ‘Absa GirlCode Hackathon 2025’, ambapo  wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali  zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia  sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.