MIMI NI BONDIA MKUBWA NDIOMAANA NILIVYOPOTEZA NIMECHEKWA NCHI NZIMA

::::::::

“Katika kipindi cha miezi kumi iliopita nimeshinda mara tatu ubingwa wa WBC Afrika. 

“Ninachotaka kusema ni kwamba kufanya kwangu vizuri kote hapo awali ukweli nikapongezwa na wachache watanzania wengi walibakia kimya lakini kupoteza kwangu juzi imekuwa sehemu ya kusemwa, kuchekwa na kuonekana siyo lolote. 

“Upande mwengine hii nimechukua kama changamoto na inanionyesha namna gani nilivyokuwa mkubwa hadi nchi imesimama kunisema kwa kupoteza pambano langu, nimeumia sana ila ahadi yangu kwenu nitarudi nikiwa bora zaidi na kufanya makubwa,” amesema Ibrahim Mafia.

Ikumbukwe Ibrahim Oktoba 10, 2025 alipanda ulingoni kwenye pambano dhidi ya mfilipino Alvin Camique ambapo alipigwa raundi ya nne na mfilipino huyo kwa ‘TKO’ kwenye pambano la raundi 10 na kupoteza pambano kwa mara ya kwanza