Na Pamela Mollel,Arusha.
Wazee wa Mkoa wa Arusha wamefanya matembezi ya amani kuadhimisha miaka 26 ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza baada ya matembezi hayo jijini Arusha katika eneo la Makumbusho,Mkuu wa Mkoa, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, aliwapongeza wazee kwa kuonesha uzalendo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025.
Makalla alisisitiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kuimarisha amani na si kusambaza taarifa za uchochezi, akibainisha kuwa “kumuenzi Baba wa Taifa ni kuendeleza misingi ya umoja, usawa na mshikamano.”
Aidha, wazee hao wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini mchango wao na kuendelea kuimarisha mabaraza ya amani pamoja na kuwahusisha katika maamuzi muhimu ya kitaifa.