Na. Vero Ignatus Michuzi Blog Arusha
Mkutano Mkuu wa 6 wa Mwaka wa AQRB 2025, umefanyika Jijini Arusha na kukutanisha taasisi za udhibiti kama AQRB, ERB, CRB,OSHA, NEMC, FIRE & RESCUE, EWURA NA TAMISEMI , Lengo kuu ni kukaa kwa pamoja na kuweza kubadilishana uzoefu katika udhibiti wa sekta ya ujenzi.
Akifungua mkutano huo wa 6 wa mwaka Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia miundombinu Rogatius Mativila ameiagiza Bodi hiyo kuboresha Mifumo ya usajili na kuhakikisha miradi yote ya Umma inasimamiwa na wataalam waliosajiliwa ili kuepusha utapeli
Ametahadharisha Bodi hiyo kuwa makini na kampuni zisizokuwa na ubora zinazojihusisha na ujenzi kudhibitiwa, kwani ubunifu mkubwa kuzingatiwa kwani yanahitajika Majengo yanayohimili mabadiliko ya tabianchi miradi ya kijani matumizi ya kisasa, Mifumo ya kidigitali katika usanifu na katika ukadiriaji wa miradi.
“Kupitia ubunifu tutaweza kujenga majengo Bora salama rafiki kwa mazingira inayoendana na ndoto ya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kidigitali” Alisema Mativila
Amewataja wakadieiaji na wasanifu Majengo kuwa ni moyo wa katika usalama wa Majengo yanayobeba maelfu ya wa Tanzania kutokana na ubora wa Majengo yanayoonyesha taswira nzuri ya nchi.
Awali akitoa salamu za Bodi hiyo Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Dkt.Daniel Matondo, amesema Bodi hiyo inasimamia uadilifu ubora na maadili ya wataalam hadi kufikia tarehe 30 Septemba 2025 wamesajili wataalam 1170 makampuni 507 kati ya januari- septemba wamefanikiwa kufanya ukaguzi wa Majengo na majenzi yaliyosajiliwa awali pamoja na yale yanayojengwa kwa sasa 4598 miradi 1276 iliyokidhi matakwa ya kisheria, aidha waendelezaji zaidi ya 103 wamefikishwa mahakamani kwa kutokufuata taratibu za kisheria.
Dkt.Matondo ameainisha mada ndogo zinazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na Taarifa za Udhibiti na Taratibu za Udhibiti wa Miradi, kuangalia mchakato wa kupata vibali na idhini kutoka Bodi na vyombo vingine vinavyohusiana na udhibiti wa miradi ya ujenzi,Mifumo ya Usalama na Afya Kazini,kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na watekelezaji wa miradi, na ufuatiliaji wa viwango vya afya kazini.
Pia watajadili Usalama wa Moto katika Miradi ya Ujenzi, kuzingatia kanuni za kujikinga na moto katika majengo na miradi ya umma na ya watu binafsi, Uendelevu wa Mazingira,Tathmini na Athari zake, kuhakikisha miradi ya ujenzi inazingatia masuala ya kimazingira na usalama wa rasilimali za taifa,Udhibiti wa Maadili na Sheria,maadili ya kitaaluma, na usajili wa wataalamu katika kuhakikisha uwajibikaji na ufanisi wa sekta,Ufuatiliaji na Ripoti za Uzingatiaji Mahiri kuangalia mbinu na zana za kuhakikisha utekelezaji sahihi wa taratibu na udhibiti katika miradi ya ujenzi. 103 wamefikishwa mahakamani kwa kushindwa kufuata taratibu za kisheria.
Vilevile, Bodi ilifanya mikutano 3 ya kinidhamu na mashauriano nawataalamu pamoja na makampuni kwa lengo la kudhibiti uadilifu na uwajibikajikatika utoaji wa huduma.Kuhusu kutoa ushauri kwa Wananchi Bodi imeshirikikatika maonesho mbalimbali yanayojumuisha wananchi kamaSabasaba,nanenane .
Aidha katika juhudi za kuongeza uelewa kwawananchi wa taaluma hizi Bodi imeendesha mashindano ya insha kwawanafunzi wa shule za msingi na Sekondari na inaanza kutoa zawadi kwawaliofanya vizuri mwishoni mwa mwezi Oktoba 2025 .
Pia Bodi imepanua wigowa matangazo kwa umma kupitia wanahabari na mitandao ya kijamii navyombo vya usafri kama SGR, Bajaj na hata katika Barua pepe za Serikali y aani GMS. AlisemaPamoja na hatua kubwa zilizopigwa katika utekelezaji wa majukumu yake,
Aidha Dkt. Matondo amesema Bodi hiyo inakabiliwa na changamoto ikiwemo: Kutokamilika kwa Sheria Majengo, jambo linalochelewesha baadhi ya taratibu muhimu za usimamizi na udhibiti katika sekta ya ujenzi Ufinyu wa bajeti ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi chini ya mpango wa AQIP, hali inayopunguza wigo wa kuwajengea uzoefu wakiutendaji wanafunzi na wahitimu Mwingiliano wa kisheria na taasisi nyingine za umma, mfano Barazal a Sanaa Tanzania (BASATA) na wadau wengine, unaohitaji uratibu .
Amesema changamoto nyingine ni pamoja na Uelewa mdogo wa Sheria ya Bodi miongoni mwa wananchi, taasisib inafsi na hata baadhi ya taasisi za umma, jambo linalosababisha changamoto katika utii na utekelezaji wa masharti yake.
Hata hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi inaendelea kutekeleza hatua za makusudi za kutatua changamoto hizi, ikiwemo kukamilisha mchakato wa Sheria ya Majengo, kuongeza ushirikiano baina ya taasisi, kuimarisha uratibu wa mafunzo kwa vitendo na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Sheria ya Bodi.
Mkutano huo wa Sita unaongozwa na Kaulimbiu isemayo: “Uzingatiaji Mahiri: Kuwawezesha Wataalamu katika Mazingira Yenye Udhibiti wa Kisheria.” Yaani kwa kiingerez Smart Compliance: Empowering Professionals in a Regulated Environment.”
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia miundombinu Rogatius Mativila
Dkt.Daniel Matondo, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB)