Meneja Mkuu wa Simba SC, Dimitar Pentev, amesema wachezaji Mohammed Bajaber na kipa Moussa Camara wataikosa mechi dhidi ya Nsingizini Hotspurs kutokana na majeraha.
Mechi hiyo ya kwanza katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kupigwa Oktoba 19, 2025 nchini Eswatini.
Pantev ametoa kauli hiyo wakati kikosi cha timu hiyo kikiondoka leo Oktoba 16, 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kuelekea Eswatini kwa ajili ya mechi hiyo.
Camara, Bajaber kuikosa Nsingizini, Meneja Pantev afichua sababu
