“Uwekezaji utaanza kwenye hisa za Benki ya CRDB, Benki ya NMB, Kampuni ya Uwekezaji ya NICO – National Investment Company Limited (NICO), Dar es Salaam Stock Exchange PLC (DSE) na Kampuni ya AFRIPRISE. Lengo la uwekezaji wa aina hii ni kuufanya mfuko huu kuwa na ukwasi wa kutosha kukidhi mahitaji ya fedha kwa wawekezaji pindi yanapotokea”.
Amesema (CMSA) ina jukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba shughuli katika masoko ya mitaji zinafanyika kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili kuleta uwazi na haki kwa washiriki wote.
“Kama tulivyoshuhudia mauzo ya vipande vya mfuko wa Vertex ETF yamepata mafanikio ya asilimia 136, ambapo kiasi cha sh billioni 6.8 kimepatikana, ikilinganishwa na lengo la sh.bilioni 5.
Aidha, asilimia 82.2 ya mauzo ya vipande imetoka kwa wawekezaji mmoja mmoja na asilimia 17.8 imetoka kwa Kampuni na taasisi.
Naye Mtendaji Mkuu wa Vertex International Securities, Mateja Mgeta, amesema wakati wanaanza kuuza vipande hivyo lengo ilikuwa kupata bilioni tano kwani kipande kimoja cha mfuko kilikuwa kinauzwa sh. 200, hadi zoezi la mauzo ya awali linakamilika waliweza kupata bilioni 6.8 Sawa na asilimia 136 na kuvuka lengo
Mgeta amesema mfuko wa ETF umeweza kupata idadi ya wawekezaji zaidi ya 6,300 na katika hao kuna wawekezaji wapya hali inayoenda sambambamba na Serikali katika masuala ya uchumi jumuishi.
“Vertex inapenda kutoa ahadi kwa Watanzania na wawekezaji wote kwa ujumla kwamba itasimamia huu mfuko kwa weledi ili kuhakikisha wawekezaji wanafaidika na matunda ya uwekezaji wao na kuendelea kuleta bidhaa bunifu sokoni zitakazokidhi mahitaji ya masoko ya mitaji na dhamana nchini.
Mgeta amesema ETF imevuka lengo na kuanzia sasa itapatikana katika soko la hisa.
Mecklaud Edson, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Peter Nalitolela amesema zaidi ya miaka 20 toka kuanzishwa kwa soka la hisa hawakuwahi kuwa na bidhaa kama hii ya Vertex.
“Tunawasihi Watanzania waje soko la hisla Dar es Salaam wataipata bidhaa hii nzuri kabisa ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa,”.