……………….
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Wakili Mwanaisha Mndeme, amefanya kikao cha ndani na wakazi wa Mjimwema ikiwa ni sehemu ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025
Katika kikao hicho, Mndeme alikutana na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo mama lishe, wajasiriamali, waendesha bodaboda pamoja na wabangua mawe, ambapo aliwasilisha vipaumbele vyake vya maendeleo ambavyo analenga kuvitimiza endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Kigamboni.
Mgombea huyo alieleza kuwa iwapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha utolewaji wa mikopo ya asilimia 10% kutoka Halmashauri inawafikia walengwa bila ubaguzi,Elimu ya ujasiriamali na elimu ya sheria kwa wajasiriamali wadogo ili kuwasaidia kufanikisha shughuli zao kwa ufanisi zaidi.
Wakazi wa Mjimwema waliipokea kwa matumaini mikakati ya Mndeme, huku wengi wakionesha kutaka mabadiliko ya kiuongozi yatakayoleta maendeleo ya kweli katika jamii yao.