MWANDISHI WA TORCH MEDIA ASHINDA TUZO ZA TMA

 :::::::::::::

Mwandishi wa habari
kutoka Torch Media, James Salvatory,  
ametunukiwa tuzo ya umahiri kwa kazi zake kuhusu hali ya hewa.

Tuzo hiyo imetolewa
leo Alhamisi, Oktoba 16, 2025, na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ikiwa
ni sehemu ya kutambua mchango wa wanahabari katika kuelimisha jamii kuhusu
mabadiliko ya tabianchi na taarifa za hali ya hewa.

Salvatory ameibuka
mshindi wa tatu katika kundi la habari za mtandaoni na kupokea tuzo hiyo kutoka
kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Jaji Mshibe Bakari.

Akizungumza baada ya
kupokea tuzo hiyo, Salvatory amesema ni heshima kubwa kutambuliwa kitaaluma, na
kwamba ushindi huo ni chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi
zaidi.

Ameongeza kuwa
uandishi wa habari za hali ya hewa ni eneo linalohitaji umakini na uelewa wa
kina, hivyo ataendelea kujifunza na kuboresha kazi zake kwa manufaa ya jamii.