Uislamu ni dini ya ulimwengu wote, inayojumuisha nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Uislamu ni imani, sharia na mfumo kamili wa maisha, unaozingatia mambo ya Kidunia na ya Akhera bila kuacha pengo lolote.
Allah Mtukufu amesema. ”Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu..” (16:89).Uislamu umeweka mwongozo wa wazi, umebainisha njia ya uongofu, na kutofautisha baina ya halali na haramu.
Wanazuoni wa madhehebu ya Kishafi wameielezea taazia: Ni kumfariji mfiwa kuwa na subira au kuutulza moyo wake, kwa kumnasihi avumilie juu ya mpendwa wake aliyempoteza, kumtia moyo kwa kumwahidi kupata thawabu, na kumtahadharisha na dhambi ya kutokuwa na subira au kulalamika, na kumuombea marehemu msamaha.
Sharia ya Kiislamu haikuamuru maneno maalumu ya kufariji, kila maneno mazuri yanayopunguza huzuni, kufariji na kutia moyo wa subira mfiwa yanakubalika, ili mradi tu yasivunje Sharia ya Kiislamu.
Ingawa bora ni kufuata muongozo wa Mtume wa Allah alipomfariji binti yake aliyefiwa na mwanawe: “Kila kitu ni cha Allah – Yeye hutwaa na hutoa Kwa mipang Yake”.
Wanazuoni wamekubaliana kuwa ni Sunna kutoa pole kwa wafiwa wote wanaume kwa wanawake, wakubwa kwa wadogo. Na wanaostahili kuzidishiwa pole wale wenye mioyo mepesi wasioweza kuvumilia msiba, na wale wenye subira ndogo au huzuni kali.
Kuna matendo ambayo Uislamu umeharamisha katika msiba, lakini bado baadhi ya watu huyafanya, miongoni mwa mambo hayo ni kulia kwa kupiga mayowe, kwa namna ya kuonesha kutoridhika na maamuzi ya Allah, kujipiga mashavu, kuchana mavazi kwa huzuni, kunyoa nywele kwa sababu ya msiba.
Lakini Sharia yaKiislamu imeruhusu kulia kimya kimya bila sautikubwa, kuchana nguo au kujipiga mashavuni. Mtume wa Allahalilia alipofiwa na mwanawe Ibrahim. Abdurrahman bin Awf (Allah amridhie) akamuuliza: “ Hata wewe Mtume wa Allah unalia!?” Akamjibu: “.. kilio hiki ni cha huruma.” akaendelea kusema: “Macho yanatoa machozi, moyo una huzunika, lakini hatusemi isipokuwa yale yanayomridhisha Mola wetu….”
Uislamu haukatazi kulia kwa huzuni ya kimaumbile; kwani kulia kwa asili yake ni jambo halali na halipingani na subira wala udhaifu wa imani.
Bottom of FormWanazuoniwa madhehebu ya Kihanafi, Malik, na wengi katika wanazuoni wa Kishafi wanaona kuwa utoaji pole kwa wafiwa uanze pale kifo kinapotokea hadi siku tatu baada ya mazishi. Baada ya hapo usitishwe kwani unaweza kurudisha huzuni.
Lakini wafuasi wengine wa madhehebu ya Kishafi na Hanbali wanaona kuwa hakunakikomo maalumu, na unaweza kufanywa hata baada ya siku zaidi ya tatu. Na hii ndio kauli yenye nguvu Kisharia.
Baadhi ya wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi, Malik na Hanbali pia ni mtazamo wa sheikh Ibin Baz –Allah Amrehemu- wameruhusu familia kukaa katika mahali maalumu kama -vile nyumbani kupokea wageni kwa ajili ya kuwafariji, lakini kwa masharti, isiwe msikitini, mbele ya mlango au barabarani au kuandaa vyakula kwa ajili ya wanaokuja kufariji.
Madhehebu ya Kishafi, Hanafi na Hanbali, pia ni mtazamo wa sheikh Ibin Uthaimin –Allah Amrehemu-. wanaona kitendo hicho ni haramu. Kauli yenye nguvu ni ya kwanza ila kama kukusanyika huko kutakuwa na mambo yaliyokatazwa Kisharia.
Uandaaji chakula kwa wafiwa
Wanazuoni wote wa Sharia ya Kiislamu wameafikiana kuwa ni Sunna kwa majirani wa wafiwa na hata familia zilizopo mbali kuandaa chakula kwa wafiwa na kuwapelekea.
Hiki ni kitendo cha watu wema kabla yetu. Kuandaa chakula kwa wafiwa ni njia ya kuonyesha upendo na kusaidia familia hiyo, kutokana na msiba na shughuli za mazishi.
Mtume wa Allah alisema “Andaa chakula kwa familia ya Jafar, kwani wamikumbwa na jambo linalowashughulisha (msiba).” Wanazuoni wa Sharia ya Kiislamu wanakubaliana kwamba ni makosa kwa familia ya marehemu kuandaa chakula kwa wageni bila sababu za msingi, kama vile mtu ambaye amekuja kumpa pole akitoka mbali na atakaa muda mrefu, na familia haiwezi kumhudumia isipokuwa kwa kuandaa chakula.
Wanazuoni wa Kiislamu wana mitazamo miwili kuhusu kumsomea marehemu Qur’an. Mosi, madhehebu ya Hanafi na Hanbali wanasema kuwa anayesoma kwa ajili ya kupata pesa, basi hakunathawabu inayoenda kwa marehemu.
Asili ya hoja hii ni kwamba kusoma Qur’an ni ibada ya mtu binafsi na haipaswi kufanyiwa kwa malipo. Hoja yao ni kauli ya Allah: “Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe? (53:39)
Pili, madhehebu ya Malik na Shafi wanasema kusoma Qur’an kwa malipo kwa muda maalumu ni halali, kwani, Kusoma Qur’an kunategemewa kutoa baraka kwa marehemu, na msomaji anaweza kumwombea marehemu baada ya kusoma na dua yake inaweza kupokelewa.
