Benki ya Absa Tanzania yazindua Klabu ya Matembezi na mbio fupi ikihamasisha umuhimu wa mazoezi kwa afya ya mwili na akili

Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia) akiwatangulia baadhi ya wafanyakazi na wateja wa kitengo cha biashar, wakati wa uzinduzi  rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja. Hafla hii ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa  Tanzania kitengo cha biashara pamoja na wateja, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi  rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja.  Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.