Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja rasmi mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Romain Folz, ambaye amejiunga na timu hiyo mwanzo wa msimu.
Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 18, 2025 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili, huku uongozi wa Yanga ukimshukuru Folz kwa mchango wake katika kipindi alichoiongoza timu hiyo.
“Uongozi wa Yanga unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya klabu yetu na unamtakia kila la heri katika majukumu yake yajayo,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa sasa, timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Patrick Mabedi, wakati mchakato wa kumpata Kocha Mkuu mpya ukiendelea.
Yanga imefikia uamuzi wa kuachana na kocha huyo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Silver Strikers ya Malawi.
Endelea kufuatilia Mwanaspoti.