Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Pwani Aongoza Wanawake Kumkaribisha Dkt. Samia Mkuranga

Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariam Ibrahim, ameongoza maandamano ya wanawake wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kumkaribisha mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maandamano hayo yamefanyika katika Kata ya Mwandege, Wilaya ya Mkuranga, utakapofanyika  mkutano wa kampeni wa Dkt. Samia.
Akizungumza wakati wa maandamano hayo, Mafuga Juma alisema kuwa wanawake wa Mkoa wa Pwani hawana muda wa kuandamana kwa maneno matupu, bali wana muda wa “kutiki” chama chao cha CCM kwenye sanduku la kura