Mwili wa Hayati Raila Odinga Wazikwa Kwa Heshima Kuu Siaya – Global Publishers



Mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Hayati Raila Amolo Odinga, umezikwa leo katika makazi yake ya nyumbani, Kang’oka Ka Jaramogi, Kaunti ya Siaya.

Mazishi hayo ya kitaifa yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wakiongozwa na Rais wa Kenya, maafisa wa serikali, viongozi wa upinzani, na wawakilishi wa mataifa rafiki.

Baada ya kushushwa kwa jeneza, mizinga 17 ya heshima ilipigwa kwa ajili ya kumuenzi Hayati Raila Odinga — ishara ya heshima kwa wadhifa aliowahi kushika kama Waziri Mkuu na mchango mkubwa alioutoa katika historia ya kisiasa ya Kenya.

Raila Odinga anakumbukwa kama mwanademokrasia, mpigania haki, na kiongozi aliyejitolea kwa maendeleo ya taifa lake.