DAKIKA ZA LALA SALAMA,DKT NCHIMBI ATUA KILWA KUSAKA KURA ZA USHINDI WA CCM.

Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi mapema leo Oktoba 20, 2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Kilwa mkoani  Lindi,ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya Kampeni ya kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Ikiwa zimebaki siku 9  za lala salama kufikia uchaguzi mkuu,Dkt. Nchimbi anatarajia kufanya mkutano wake wa hadhara wa kampeni wa kunadi Sera na Ilani ya CCM (2025-2030) katika kata ya Tingi, jimbo la Kilwa  Kaskazini na kuomba  ridhaa ya wananchi kukipigia kura za ndio chama hicho kupitia wagombea wake katika nafasi zote kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.