MSADO ATAKA SUALA LA POLEPOLE WAACHIE VYOMBO VYA DOLA

………………….

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, Wakili Albert Msando ametaka suala la kupotea kwa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini CUBA, Humphrey Polepole liachiwe vyombo vya dola vifanye uchunguzi na kuja na taarifa kamili.

Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya amesema hakuna anayejua kama ni kweli Polepole alikuwa nchini au la kutokana na kauli zake.

“Sasa hivi kumezuka tabia kwa baadhi ya watu wanaofanya uharifu wakikamatwa wanaodai wametekewa, tuache hizi tabia na tuviachie vyombo vya dola vitoe taarifa kamili badala ya kila mtu kuwa msemaji.

Msando ametoa mfano wa kiongozi mmoja wa dini aliyeokotwa porini jana ambako awali taarifa zilienezwa kuwa ametekwa.

Mkuu huyo wa wilaya  amewataka  wakazi wa Ubungo kujitokeza Kwa wingi siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 na kumchagua kiongozi waneyemtaka badala ya kusikiliza maneno ya upotoshaji yanayoandikwa katika mitandao ya kijamii 

Msando ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2025 wakati akiwa mgeni rasmi katika kongamano la Shirikisho la wana Vicoba Jijini Dar es Salaam (VICOBA FETA).