RC CHALAMILA ARUDISHA TABASAMU KWA MJANE BI ALICE HAULE

………………….

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amehitimisha mgogoro wa nyumba kiwanja namba 819 Msasani beach uliomhusisha mjane wa marehemi Justice Rugaobula, Bi Alice Haule na Muhammed Mustafa Yusuf Ali ambapo amemkabidhi hati maalum iliyotolewa na wizara ya Ardhi ambayo inamtambilisha Bi Alice Haule ndiye msimamizi halali wa mirathi kisheria baada timu ya wataalamu aliyoiunda kujiridhisha kuwa mjame huyo ndiye anaepaswa kukabidhiwa umiliki wa nyumba hiyo kama msimamizi wa mirathi

Akizungumza leo Octoba 20,2025 Jijini Dar es Salaam RC Chalamila amesema baada ya kuibuka kwa mgogoro huo wa nyumba aliamua kuunda timu maalum ya wataalamu iliyohusisha wataalamu kutoka ofisi ya kamishna wa ardhi, jeshi la polisi na mawakili kutoka pande zote za mgogoro ambapo timu hiyo imejiridhisha kuwa Bi Alice ndio mwenye haki kwenye nyumba hiyo kama msimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe bwana Justice Rugaobula

Aidha RC Chalamila baada ya kumkabidhi hati miliki iliyoandikwa jina lake Bi Alice kama msimamizi wa mirathi amemkabidhi pia mjane huyo kiasi cha shilingi milioni 10 kama kifuta machozi kitokana na usumbufu alioupata na amemtaka Muhammed Mistafa Yusuf Ali kufika ofisini kwake ndani ya muda wa siku tano kwani muda wote wa kuendesha shauri hilo amekua akitafutwa na hajawahi kutokea lakini pia anatuhuma za kutumia vibaya majina ya viongozi

Kwa upande wa Naibu Kamishna wa ardhi Mkoa wa Dar es salaam Shukrani Kyando akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya ardhi ameeleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa hadi kufikia maamuzi ya kumkabidhi nyumba hiyo Bi Alice ambapo amesema nyumba hiyo haikuuzwa kisheria kwani fedha walizopeana ni za kukopeshana lakini pia hakuna sehemu Bi Alice alishiriki uuzaji wa nyumba hiyo ya wanandoa

Mara baada ya maamuzi hayo kitolewa Bi Alice kukabithiwa hati miliki ya nyumba hiyo mjane huyo amemshukiru Rais Dkt Samia na Mkuu wa mkoa Dar es salaam kwa kumuwezesha kupata haki hiyo na amebainisha kuwa kwa sasa anaishi na watoto wanne wawili amezaa na marehemu mumewe lakini wawili ni watoto wa mrehemu mumewe aliozaa na mwanamke mwimgine