:::::::
Bondia Mtanzania, Ezra Paul amefuzu hatua ya fainali kwa kumtandika kwa ‘points’ mpinzani wake raia wa Rwanda, Murenzi Hassan.
Paul amemtandika Hassan kwa ‘ponts’ 5-0 katika pambano la hatua na nusu fainali ya mashindano ya ngumi barani Afrika ambayo yanafanyika nchini Kenya jijini Nairobi.
Fainali ya michuano hiyo itafanyika siku ya Ijumaa jijini Nairobi.