Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki Ibada Maalum ya kumuombea aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Marehemu Dkt. Stephen Munga, iliyofanyika Maramba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
Ibada hiyo imeongozwa na Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Askofu Maimbo Mndolwa na kuhudhuriwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa, Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga Mhashamu Thomas Kiangio, Katibu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga Sheikh Muhsin Mohamed pamoja na waumini mbalimbali.
Akizungumza na waumini baada ya Ibada hiyo, Makamu wa Rais amesema ushirikiano baina ya Serikali na Taasisi za dini ni muhimu sana kuendelea kudumishwa. Amewasisitiza viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa salama na lenye amani pamoja na kuwaombea viongozi waweze kufanya kazi kwa mapenzi ya Mungu kwa faida ya wananchi.
Aidha Makamu wa Rais amewasihi wananchi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi wa Oktoba na kuhakikisha amani inadumishwa wakati na baada ya uchaguzi. Amesema shughuli zote za kijamii na kiuchumi ikiwemo kufanya ibada zinafanyika vema kutokana na amani iliyopo.
Askofu Mstaafu, marehemu Dkt. Stephen Munga alifariki tarehe 20 Septemba 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa dini mara baada ya kuwasili Maramba mkoani Tanga kushiriki Ibada Maalum ya kumuombea aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Marehemu Dkt. Stephen Munga, iliyofanyika, Maramba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha maombolezo wakati alipowasili nyumbani kwa aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Marehemu Dkt. Stephen Munga, kushiriki Ibada Maalum ya kumuombea Askofu huyo, Maramba mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada Maalum ya kumuombea aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Marehemu Dkt. Stephen Munga, iliyofanyika, Maramba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Marehemu Dkt. Stephen Munga wakati wa Ibada maalum ya kumuombea Askofu huyo, iliyofanyika, Maramba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakifanya maombi pamoja na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga Mhashamu Thomas Kiangio mara baada ya Ibada Maalum ya kumuombea aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Marehemu Dkt. Stephen Munga, iliyofanyika, Maramba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.