Mabao mawili ya mshambuliaji Jeremiah Juma na winga Haruna Chanongo yametosha kuipa ushindi wa mabao 2-1 Tanzania Prisons dhidi ya watani zao Mbeya City katika mchezo wa Dabi ya Mbeya uliopigwa jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo wa mchezo wa Ligi Kuu Bara unaifanya Prisons kushinda mchezo wake wa kwanza ugenini baada ya kupoteza miwili ugenini na kushinda mmoja kwenye mechi zake nne ilizocheza.
City wamepoteza mchezo wa kwanza nyumbani msimu huu, wakishinda miwili na kupoteza mmoja ugenini, huku wakitokaa sare mara moja nyumbani.
Kipindi cha kwanza kimemalizika bila timu yoyote kupata bao na umakini kwenye eneo la mwisho la kumalizia ukizigharimu timu zote mbili kutopata chochote.

Mashabiki wachache majukwaani kwenye Uwanja wa KMC wamelazimika kusubiri hadi dakika ya 72 kuona bao la kwanza mfungaji akiwa Jeremiah kwa shuti kali akipokea pasi ya Michael Mutinda lililomshinda kipa Benno Kakolanya.
Wakati Mbeya City wakijiuliza wakajikuta wanaruhusu bao la pili mfungaji akiwa Chanongo kwa shuti kali tena akipokea pasi ya Henry Onyango.
Ushindi huo unaifanya Prisons kupaa mpaka nafasi ya tano kutoka ile ya 13 ilikokuwa ikifikisha pointi sita baada ya kucheza mechi tano, huku City ikibaki na alama saba katika msimamo wa ligi hiyo.