::::::
Nahodha wa timu ya ngumi ya Taifa ya Tanzania kwa upande wa wanawake Zulfa Macho ameingia hatua ya fainali ya michuano ya ngumi barani Afrika inayofanyika nchini Kenya.
Macho amemtandika kwa ‘points’ 5-0 mpinzani wake bondia kutoka nchini DR Congo, Deborah Bawo katika mashindano hayo ya kanda ya tatu yanayoendelea jijini Nairobi katika uwanja wa ndani wa Kasarani.