::::::::
Mabondia nane kutoka Tanzania wakiongozwa na Yusuf Changalawe pamoja na Kassim Mbundwike watapanda ulingoni leo katika hatua ya nusu fainali ya pili mashindano ya ngumi barani Afrika kanda ya tatu yanayofanyika nchini Kenya.
Changalawe atamenyana na Fotouo Totap Jr kutoka Cameroon katika uzani wa Light Heavyweight (80kg), huku Mbundwike, ambaye alipita moja kwa moja baada ya mpinzani wake kutoka DR Congo kujiondoa hatua ya robo fainali, akikabiliana na Alvine Odour kutoka Kenya B katika uzani wa Light Middleweight (71kg).
King Lucas, baada ya ushindi wake wa robo fainali, atapambana na Maniloba Farahat wa Uganda katika uzani wa Light Welterweight (63.5kg), wakati Azizi Chala, aliyewadhibu wapinzani kutoka DR Congo, atamenyana na Issouhou Mouhaman wa Cameroon.
Kwa upande wa wanawake, Zulfa Macho atapanda ulingoni dhidi ya Bisambu Deborah wa Uganda katika Bantamweight (54kg), huku Aisha Iddi “Shisha” akimenyana na Muduwa Brenda wa Uganda katika Light Flyweight (50kg).
Vumilia Twalibu (Lightweight – 60kg) atapigana na Munga Zalia kutoka DR Congo, na Rachel Msengi (Light Heavyweight – 81kg) kutoka Dodoma atakabiliana na Lorna Kusa wa Kenya A.
Mashindano hayo hayo yanafanyika katika uwanja wa ndani wa Kasarani uliopo jijini Nairobi.
Kutoka juu kushoto: Azizi Chala, Zulfa Macho, King Lucas, Yusuf Changalawe, na Kassim Mbundwike.
Mungu wabariki Faru Weusi, Mungu ibariki Tanzania