Mahakama Kuu yakubali pingamizi la Lissu

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, imekubaliana na pingamizi la Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu na kukataa kupokea flash disk na memory Card kwa maelezo kuwa shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Samwel Kaaya(39) sio mtaalamu wa picha za mjongeo (video) na badala yake ni mtaalamu wa picha mnato.

Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatano Oktoba 22, 2025 na kiongozi wa jopo la majaji watatu, Jaji Dustan Nduguru, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Lissu aliwasilisha sababu nne mahakama hapo akipinda shahidi huyo kutoa kielelezo hicho mahakamani hapo kwa madai kuwa hana sifa za kutoa kielelezo hicho.

Endelea kifuatilia mitandao ya kijamii.