Ubiasafari yaja na mbinu ya kuondoa foleni katika jiji la Dar es Salaam

Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Ubia Safari Inayojishughulisha na kulaza magari makubwa ya mizigo imesema kuwa umeamua kuja na njia ya kuondoa changamoto foleni kati ya jiji la Dar es Salaam kwa kuweka maeneo mbalimbali ya kulaza magari magari makubwa.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Victor kulaza Kabegu amesema kuwa Kampuni hiyo imekuja kutatua tatizo la foreni ya magari makubwa ya mizigo barabarani wakati yanapokua yametoka kupakia mizigo bandarini na maeneo mengine.

Amesema kuwa magari hayo wanaegesha sehemu yeyote na kufanya jiji kuwa na foleni na wakati mwingine yanaonekana yamepata hitilafu kumbe ni kutaka kuegesha.

“Awali kuna baadhi ya viongozi wa Serikali waliwahi kugusia kuwapo kwa tatizo hili la magari makubwa ya mizigo kutokuwa na maeneo maalum ya kuyaweka au kulaza jambo ambalo pia husababisha foleni kubwa barabarani kwani hulazimika kuegesha sehemu yeyote ,” alisema

Mkurugenzi Kabegu amesema Kampuni kuona magari mengi yako katika barabara za watembea kwa miguu na wakati mwingine magari hayo yako katika vituo vya abiria wakaamua kufanya suluhisho hilo ikiwa ni kuondoa foleni na kusababisha baadhi ya shughuli kuwachelewesha wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine

Kampuni hiyo imeweza kuwarahisishia wamiliki au madereva kuwa mfumo kwa njia ya mtandao jambo linalosaidia kwa asilimia kubwa kupungua kwa foleni barabarani.

Alisema kuwa kuwepo kwa maeneo hayo ya kulaza au kuegesha magari makubwa ya mizigo kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ajira kwa vijana katika kufanya shughuli mbalimbali kwenye magari.

“Kampuni tangu kuanza kutoa hudma wameweza kuzalisha ajira kwa vijana zaidi ya mia tano (500) wa kitanzania kwani vijana hawa wanajishughulisha na baadhi ya kazi za Ulinzi , ufundi wa magari, kukusanya ushuru na bado tunaendelea kutengeneza ajira nyingine nyingi zaidi,” alisema