OSHA yadhamiria kuongeza uelewa wa wadau kupitia vyama vya wafanyakazi

Na mwandishi Wetu

Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa Mkoa wa Dar es Salaam wapatao 180 wamepatiwa mafunzo ya awali ya usalama na afya mahali pa kazi ili kuwawezesha kuzishauri menejementi za Taasisi zao kuboresha mazingira yakazi na hivyo kupunguza ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

Mafunzo hayo yaliyowahusisha wenyeviti na makatibu wa matawi yote 90 ya TUGHE yaMkoa wa Dar es Salaam, yamefanyika katika kikao kazi cha siku mbili (Oktoba 21 na22, 2025), Kibaha Mkoani Pwani ambapo viongozi wapatao 180 wameshiriki.

Pamoja na masuala mengine, mada mbalimbali zinazolenga kujenga uelewa wa jumlakuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi zimewasilishwa na wataalam waOSHA. Mada hizo ni pamoja na; Dhana ya Usalama na Afya mahali pa kazi, Uwakilishina Kamati za Afya na Usalama mahali pa kazi, Mifumo ya Usalama na Afya mahali pa kazi pamoja na misingi ya huduma ya kwanza mahali pa kazi.

Wawasilishaji wa mada kutoka OSHA, Bw. Simon Lwaho na Moteswa Meda wamesisitiza washiriki kuwahamasisha wafanyakazi wenzao katika sehemu za kazikujifunza kanuni bora za usalama na afya kutegemeana na shughuli zao za kila siku ilikupata mbinu za kujilinda dhidi ya vihatarishi mbalimbali vya magonjwa na ajali mahalipa kazi.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha kikao kazi cha viongozi hao, Mtendaji Mkuuwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, aliyekuwa Mgeni Rasmi wa hafla ya kufunga kikao kazi hicho, amesema viongozi hao wanayo nafasi muhimu katika kushawaishi menejimenti za Taasisi zao kuboreshamazingira ya kazi ili kuleta ustawi wa wafanyakazi.

“Kupitia kikao kazi hiki tumewaeleza wenzetu wa TUGHE jitihada za serikali katikakuimarisha afya, usalama na ustawi wa wafanyakazi ambapo mbali na kuiwezeshaOSHA kusimamia uzingatiaji wa taratibu za usalama na afya, masuala hayayamejumuishwa katika kanuni za kudumu za utumishi wa umma. Aidha, uzingatiaji wamasuala ya usalama na afya unaangaliwa katika ukaguzi wa CAG pamoja na Tume yaUtumishi wa Umma,” ameeleza Mtendaji Mkuu wa OSHA.

Aidha, Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA nchini, Bi. Mwenda, ameahidi kuendeleakushirikiana na TUGHE pamoja na vyama vingine vya wafanyakazi katika kuhakikishakwamba wafanyakazi nchini wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na kanunibora za usalama na afya zitakazowawezesha kutekeleza majukumu yao ya msingikatika hali ya ya usalama na kubakia na afya njema.

Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Komredi Brendan Maro ameielezeaOSHA kama mdau muhimu katika utekelezaji majukumu ya chama chao.

“Tunawashukuru sana OSHA kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakitupatia katikautekelezaji wa majukumu yetu hususan suala la kutoa elimu kwa wanachama wetuambao ni wafanyakazi,” amesema Komredi Maro.

Akitoa neno la shukrani, mwakilishi wa washiriki wa mafunzo hayo, Bi. Norbetha Sanga ambaye ni Katibu wa TUGHE Tawi la Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) amesemamafunzo ya usalama na afya ni muhimu kwa wafanyakazi na waajiri ili kuwa nauzalishaji wenye tija.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akiwasilisha hotuba yake katika hafla yakuhitimisha kikao kazi cha siku mbili cha viongozi wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Kibaha Mkoani Pwani.

Mwenyekiti na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam (Brendan Maro na Sara Rwezaula-Kulia) wakimpokea Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, alipowasiliKibaha, Pwani kwa ajili ya kufunga kikao kazi cha Viongozi wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la OSHA, Bi. Beatrice Lengereri.

Mkufunzi wa OSHA, Bw. Simon Lwaho, akiwasilisha mada kuhusiana na masuala yausalama na afya kazini katika kikao kazi cha viongozi wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza wa OSHA, Bi. Moteswa Meda, akiwasilisha madakuhusiana na Misingi ya Huduma ya Kwanza mahali pa kazi katika kikao kazi cha viongozi wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Viongozi wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali kuhusianana masuala ya usalama na afya mahali pa kazi katika kikao kazi chao kilichofanyikaKibaha Mkoani Pwani.

Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la OSHA, Bi. Beatrice Lengereri akiwa sambamba nawenyeviti na makatibu wa matawi mbalimbali ya TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, wakifuatilia mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama na afya mahali pa kazikatika kikao kazi chao kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja nawenyeviti na makatibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuhitimishakikao kazi chao kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Zoezi la uchunguzi wa magonjwa yatokanayo na kazi likiendelea kufanyika kwaviongozi wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam ambao wameshiriki kikao kazi cha siku mbili cha chama hicho Kibaha Mkoani Pwani.