::::::::
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kuzungumza na mabalozi wa nchi zisizo wanachama wa Umoja wa Ulaya (Non-EU Ambassadors) waliopo nchini, kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kujadili maeneo ya ushirikiano wa pamoja.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mabalozi kutoka Norway, Switzerland, Uingereza na Canada.