Dar wa Salaam. Lengo kuu la sharia ya Kiislamu ni kutimiza manufaa na kuzuia madhara. Sharia hii tukufu imehakikisha haki za watu binafsi na jamii nzima za kibinadamu.Β
Miongoni mwa uzuri wa sharia ya Kiislamu ni kulinda haki za wanyonge, ikiwemo makundi maalumu kama watoto.Β
Kwa ajili yao, Uislamu umeweka kanuni za jumla pamoja na sharia maalumu zenye maelezo ya kina, ikiwemo sharia za ulezi na utunzaji wa matoto (Al-Hadhana).Β
Malezi katika Uislamu ni miongoni mwa mambo mazuri sana yaliyomo katika sharia hii tukufu.
Wanazuoni waΒ Sharia ya Kiislamu (Fuqahaau) wa zamani na wa kisasa wametofautiana katika kueleza maana yaΒ malezi (Al-Hadhana) kwa maneno, ingawa maana yao kimsingi ni moja. Baadhi ya wanazuoni wa KishafiΒ wameyaelezea malezi kuwa ni kumuangalia na kumtunza yule asiyeweza kutofautisha mambo au kujisimamia, kwa kumlea kwa yale yanayomfaa, na kumlinda dhidi ya mambo yanayoweza kumuangamiza.
MaleziΒ na utunzaji wa mtoto mdogo na kusimamia mambo yake ni jukumu la wajibu la wazazi wawili wanapokuwa bado katika ndoa.
Β Ila mama ana nafasi kubwa zaidi katika haki ya malezi, kwani mara nyingi ndiye anayebeba jukumu la malezi kwa huruma na upendo. Baba naye ana nafasi, lakini ni ndogo zaidi kulingana na wajibu wa kijinsia na kimaumbile. Allah Mtukufu ameutaja wajibu huu ndani ya Qurβan: βNa useme: Ee Mola wangu, warehemu wazazi wangu kama walivyonilea utotoni.β (17:24).Β
Aya hii tukufu imeonesha wazi kuwa malezi ni jukumu la lazima la wazazi katika kipindi cha utotoni.Β
Hata hivyo, iwapo wazazi watatengana, suala la nani anayepewa haki ya kulea mtoto linaibuka: je, ni mama au baba? Na je, haki hiyo inamhusu mtoto wa kiume au wa kike?
Haki ya malezi kipindi cha talaka
Malezi na utunzaji wa mtoto unakuwa kwa wazazi wote wawili iwapo ndoa yao bado ipo. Lakini wakitengana kwa talaka, basiΒ ulezi wa mtoto unakuwa ni haki ya mama na jukumu la baba ni kuhudumia kwa makubaliano ya wanazuoni wote, kwa mujibu wa kauli ya Mtume ( Rehema na amani ziwe juu yake) aliyomwambia mwanamke aliyetalikiwa, na mtalaka wake akataka kumchukua mtoto aliyezaa naye: βWewe (mke) una haki zaidi ya kumlea mtoto, maadamu hujaolewa.βΒ
Hivyo, kauli hii ya Mtume wa Allah ni hukumu ya lazima inayopaswa kutekelezwa. Iwapo mama ataolewa na mume mwingine ambaye si baba wa mtoto, basi haki hii ndio itaondolewa kwake..Β
Imamu Bukhari β Allah amrehemu- amenukuu Hadithi ya Al-Barrau bin Azib kuhusu haki ya kumlea binti wa Hamza (Allah Amridhie). Ali (Allah Amridhie) alisema: βMimi nina haki zaidi naye, kwani yeye ni binti wa ami yangu. Huku JafarΒ akisema: βNi binti wa ami yangu, na mama yake mdogo ni mke wangu.β Zaid nayeΒ akasema: βYeye ni binti ya ndugu yangu.βΒ
MtumeΒ wa Allah akamhukumia mtoto huyo kwenda kulelewa kwa mama yake mdogo akasema: βMama yake mdogo ni kama mama mzazi.β Hadithi hii inaonyesha uhalali waΒ malezi kwa mama mdogo, na kwamba katika mgogoro anapewa kipaumbele kuliko ndugu wengine wa karibu wa mtoto.
Β Aidha, miongoni mwa athariΒ na kauli za Masahaba wa Mtume zilizopokewa kuhusu jambo hili ni simulizi inayo muhusu Umar bin al-Khattab (Allah amridhie), ambaye alimtaliki mke wake wa Kiansar baada ya kuzaa naye mtoto aitwaye Asim.Β
Baada ya mwanamke huyo kuolewa tena na mume mwingine, mtoto alilelewa na bibi yake mzaa mama. Umar (siku moja) alipokutana na mtotoΒ wake barabarani, alimkumbatia kwa mapenzi, lakini bibi yake (mzaa mama) alizozona na Umar na kumdai mtoto huyo.
Wakapeleka shauri hilo kwa khalifa (kiongozi) Abubakr as-Siddiq (Allah amridhie), naye akamhukumia mtoto abaki kwa bibi yake mzaa mama.
Miongoni mwa sharti ya mlezi: Mosi, awe mtu mzima, kwani mtoto mdogo hawezi kumlea mwenzake. Pili, awe na akili timamu. Tatu, awe na uwezo wa kulea vizuri Nne, awe mwadilifu na mwaminifu katika malezi.Β
Tano,uislamu wa mlezi si sharti la msingi katika malezi; kwa sababu huruma ya asili kwa mtoto haipotei kwa tofauti ya dini. Ila kama kuna hofu kwamba mtoto ataathiriwa na ibada za dini nyingine.
Wanawake kwa ujumla wana haki zaidi ya malezi kuliko wanaume, na malezi hayo huanza tangu kuzaliwa kwa mtoto. Hata hivyo, muda wa kumalizikaΒ Β kwa wanawake baada ya wanandoa kuachana, unatofautiana kati ya madhehebu ya Kiislamu.Β
Kwa mujibu wa madhehebu ya Kishafi, malezi huendelea kwa mtotoΒ awe wa kiume au wa kike hadi anapofikia umri wa kutambua mambo (utambuzi).
Β Umri huu unakadiriwa kuwa kati ya miaka saba hadi minane kwa kawaida. Mtoto akifika umri huu, hupewa haki ya kuchaguaΒ kuishi na mmoja kati ya wazazi wake; akimchagua mmoja, basi hukabidhiwa kwake.
