Kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Silver, mageti yatafunguliwa saa 4:00 asubuhi na kufungwa saa 8:30 mchana.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema sababu ya kufungua mageti mapema ni kuepuka msongamano wakati wa kuingia kutokana na kuamua kutoa fulsa kwaashabiki wa timu hiyo kuingia bure.
“Tumewasiliana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wamiliki wa uwanja na kukubaliana kufungua mageti mapema na kufunga muda mchache kabla ya mechi ili kuepusha msongamano wa kuingia kwa timu,” amesema Kamwe.
“Wanachama na mashabiki wa timu yetu kwa ujumla na wapenzi wa soka wajitoleze kwa wingi mapema ili kuepuka changamoto ya msongamano lakini nawaahidi kuwa kwa muda huo wa mapema watakaoingia uwanjani kutakuwa na burudani kutoka kwa ma-DJ mbalimbali.”
Kamwe amesema licha ya kutangazwa kuwa mashabiki wataingia bure viwanjani kutakuwa na utaratibu wa kugawa tiketi kwa mashabiki ambazo ndio zitawaruhusu kuingia ndani.
Pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba mashabiki watakao jitokeza kushuhudia mchezo huo kuwa waungwana ili kuepuka vurugu ambazo hazitakuwa za kiungwana michezoni na kujiingiza kwenye shida na Shirikisho la Soka Tanzania TFF na CAF.
