Mabedi: Njoo muone, Yanga ipo tayari

KAIMU kocha Mkuu wa Yanga, Patrick Mabedi ambaye ni raia wa Malawi, amesema ushindi dhidi ya Silver Strickers ni muhimu ili kuhakikisha timu inatinga hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF), mwaka huu.

Mechi ya ugenini iliyopigwa Oktoba 18 Yanga ilifungwa kwa bao 1-0  dhidi ta Silver timu ilikuwa chini ya Folz kama koma kocha mkuu na Mabedi msaidizi, ambapo kesho Jumamosi atasimama benchi akiwa kaimu kocha mkuu.

“Ni mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kuingia hatua ya  makundi, wachezaji wapo tayari kwa kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki,” amesema kocha na kuongeza:

“Yanga ni klabu kubwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuyapindua matokeo ya kufungwa ugenini na kushinda nyumbani.”

Amesema baada ya kutua nchini Jumatatu wakitokea Malawi walianza mazoezi Jumanne na kufanyia kazi upungufu, na kwamba kwa  sasa wapo tayari kukabiliana na wapinzani wao.

“Katika mpira wa miguu kila mechi ina presha yake, lakini hilo haliniogopeshi kwa sababu nimetoka timu yenye presha, naamini kila kitu kesho kitakwenda sawa,” amesema.

MABE 01

Kocha wa Silver Strickers, Etson Kadenge amesema anafahamu anakutana na Yanga yenye wachezaji bora, lakini kwa upande wao wapo tayari kumalizia dakika 90 za uamuzi wa kufuzu hatua ya makundi na kwamba anatarajia mchezo mzuri na wa ushindani huku akisisitiza kuwa wamekuja kushindana ili kufuzu.

“Wachezaji wangu wapo tayari na wameahidi kutumia dakika 90 kushindana na Yanga kupata nafasi ya kufuzu hatua inayofuata wanatambua wanakutana na wapinzani bora ambao pia wanataka matokeo ili kutinga hatua inayofuata,” amesema.