:::::::::
Mabondia saba wa Tanzania wamepata medali za fedha na shaba hadi sasa katika mashindano ya ngumi barani Afrika yanayoendelea hapa nchini Kenya.
Kipindi cha kwanza cha mashindano hayo tayari kimemalizika hapa katika uwanja wa ndani wa Kasarani jijini Nairobi na wachezaji wa timu ya Taifa ya ngumi kutoka Tanzania wakitwaa medali hizo.
Mabondia wafuatao kutoka katika timu ya Taifa ya Tanzania ndio wametwaa medali hizo.
1 Zulfa Macho – medali ya fedha
2 Salma Yahya – medali ya fedha
3 Veronica Ebron – medali ya fedha
4 Veronica Patric – medali ya shaba
5 Salma Changarawe – medali ya shaba
6 Aisha Iddy – medali ya shaba
7 Vumilia Twalib – Medali ya shaba
Mashindano bado yanaendelea hapa Nairobi.