Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ametoa tahadhari kwa mashabiki wa soka nchini, kuelekea kwenye mechi kubwa zitakazochezwa mwishoni mwa wiki zikizihusisha Klabu za Yanga na Simba.
Amesema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha usalama unaimarishwa na kueleza kuwa, kwenye Mechi ya Yanga dhidi ya Silver Strikers, mashabiki wanatakiwa kuelewa kwamba mechi ya soka ina matokeo matatu, kushinda, sare au kufungwa na kwamba katika hali yoyote, mashabiki wanatakiwa kufuata sheria.
Related