Watatu kutoka kushoto ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato kusini, Paschal Lutandula.
…………
CHATO
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chato kusini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Paschal Lutandula, amesema haendi Bungeni kutafuta pesa bali kupata ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo.
Amewataka wamuamini na kukiamini Chama Cha Mapinduzi kuwa kina lengo la kuwaletea maendeleo wananchi na siyo vinginevyo.
“Naomba Oktoba 29 mwaka huu kwa wingi wenu mwende kuwapigia kura nyingi wagombea wa CCM kuanzia Rais, mimi mwenyewe ili niwe Mbunge na Diwani wa kata ya Nyarutembo mumchague Majebele”.
Amesema anayo dhamira njema ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Chato kusini ili kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na keki ya taifa badala ya watu wachache.
“Niambieni wananchi wa Nyantimba mnataka nini, nia yangu ni moja na nia yangu ni njema ya kuwaletea maendeleo ya kweli, nimeshaahidi kuwa nitakuwa mtumishi wenu mwaminifu na wala sitobadilika”,
“Naimbeni mumuamini mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, mniamini na mimi pamoja na CCM kuwa tumekusudia kuwaleteeni maendeleo na kuondoa kero zenu za muda mrefu” amesema Lutandula.
Amesisitiza kuwa hatokuwa Mbunge wa kusinzia Bungeni ispokuwa kuwapambania wananchi wa Jimbo la Chato kusini ili waboreshe uchumi wao kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
“Nawaahidi wananchi mkinichagua kuwa Mbunge wenu sitawaangusha, nitafanya kazi usiku na mchana ili kuwatumikieni ninyi, wala siendi Bungeni kutafuta pesa ila kwenda kumaliza kero zenu” amesema.
Hata hivyo ameahidi kupeleka umeme kwenye makarasha ya kusaga mawe ya dhababu ili iwe rahisi kwa wachimbaji madini kuzalisha kwa njia nyepesi ukilinganisha na sasa ambapo wanatumia mitambo ya mafuta ambayo inawagharimu pesa nyingi.
Β Kadhalika katika uongozi wake amedai atahakikisha vinachimbwa visima virefu na vifupi ili kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu na gharama za kutibia magonjwa yatokanayo na kunywa maji machafu.
Β Β Β Β Β Β Β Β Β Β Β Mwisho.


