Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelealo (Chadema), Tundu Lissu amefikishwa tena katika Mahakama Kuu leo Oktoba 24, 2025 ikiwa ni mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili.
Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani iliyopelekwa kwa pande zote, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mfululizo kuanzia Oktoba 6, mpaka leo Oktoba 24, 2025.
Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Endelea kufuatilia Mwananchi

