Mgombea wa Urais Zanzibar, Othman Masoud, Afunga Kampeni Pemba – Global Publishers



 

Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Ndugu Othman Masoud.

Kampeni za mgombea wa Urais wa Zanzibar, Ndugu Othman Masoud, Kisiwani Pemba zimefungwa zikihudhuriwa na wafuasi wengi na viongozi wa ndani ya Chama chake.

Akizungumza katika hafla hiyo, Othman Masoud alisisitiza:

“Vile tulivyofunga kampeni Kisiwani Pemba ni ishara ya mshikamano wetu. Ushirikiano wenu na hamasa yenu ni nguvu yetu. Tuwe pamoja katika kujenga Zanzibar yenye maendeleo na amani.”

Mgombea pia aliwashukuru wafuasi wake kwa ushirikiano, hamasa, na imani waliyoonyesha katika kipindi chote cha kampeni, na kuwaomba kuendeleza amani na mshikamano wa kijamii hadi siku ya uchaguzi.