TMA YATANGAZA TAHADHARI YA MVUA KUBWA JUMATATU NA JUMANNE


::::::

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kesho katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (pamoja na visiwa vya Mafia), Morogoro na Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, hali kama hiyo pia inatarajiwa kuendelea hadi keshokutwa (Jumanne) katika mikoa hiyo na kuongezeka hadi maeneo ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Mamlaka imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa zitakazotolewa ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.